Friday 27 April 2018

Marais wa Korea Kaskazini.na kusini kukutana



Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un anatarajia kukutana ana kwa ana na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in siku ya leo Ijumaa  Aprili 27, 2018

Rais wa Korea Kaskazini anatarajiwa kuwa Kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo kuingia nchini Korea Kusini tangu kumalizika vita vya Korea, mwaka 1953

Mazungumzo hayo ya kihistoria yatalenga nia ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini ya kuachana na silaha za nuklia. Lakini ugumu unakuja kuwa ni kwa kiasi gani watafikia makubaliano

Aidha, viongozi hao pia wanatarajiwa kujadili njia za kupata amani katika eneo la Peninsula na kuhitimisha rasmi vita vya Korea vya mwaka 1950-1953 na maswala ya uchumi na kijamii

0 comments:

Post a Comment