Sunday 29 April 2018

Mtoto wa rais Guinea akamatwa kwa kufanya utumwa Marekani



Mtoto wa Rais wa Guinea, Ahmed Sékou Touré pamoja na Mkewe washtakiwa kwa tuhuma za kumfanya Msichana mmoja mtumwa wao kwa miaka 16

Mohamed Touré pamoja na Mkewe Denise Cros-Touré, wote wenye umri wa miaka 57 wanatuhumiwa kwa kumchukua msichana huyo nchini kwao Guinea na kumpeleka kwenye makazi yao huko Texas, Marekani akiwa na umri wa miaka 5 tu

Wawili hao wameshatakiwa kwa tuhuma za utumikishaji wa Watoto na endapo watakutwa na hatia watakabiliwa na kifungo cha mpaka miaka 20 jela

Msichana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa amefanikiwa kutoroka kwa msaada wa majirani

0 comments:

Post a Comment