Monday 27 November 2017

Tahadhari yatolewa baada mlima wa volkano kulipuka

Mamlaka nchini Indonesia imetangaza hali ya tahadhari kufuatia kuwepo dalili za kutokea mlipuko mkubwa wa Volcano katika mlima wa Agung.
Huku uwanja unaotumika jijini hapo ukiwa umefungwa kutokana na tahadhari ya kupata ajali kwa ndege kutokana na mlipuko huo.
Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3000 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza.

Mlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.
Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama ene hilo na kwenda kwingine.
Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600.

0 comments:

Post a Comment