Serikali ya India imepiga marufuku wanafunzi wa mji wa #Biar kuvaa soksi na viatu kwenye vyumba vya mitihani ili kuzuia kupiga chabo na kuficha majibu.
Wanafunzi wa mji huo watafanya mitihani ya kumaliza darasa la kumi wakiwa peku pamoja na kufanyiwa ukaguzi mwilini na kutakua na CCTV camera katika vyumba vya mitihani kuanzia February 21.
Mwaka 2016 mji wa Biar uliweka sheria ya kulipa faini na adhabu za jela kwa wanafunzi watakaobainika kufanya udanganyifu baada ya mwanafunzi aliyeongoza kufanya vizuri kubainika aliingia na majibu kwenye mitihani na kufeli aliporudia mitihani aliyofaulu mara ya kwanza.
Mwaka 2013 walikamatwa wanafunzi 1,600 kwa kupiga chabo kwenye mitihani pamoja na wazazi 100 walihusika kuwapa mbinu watoto za kuibia majibu kwenye mitihani.
By @racathedon | Source ; BBC
0 comments:
Post a Comment