Saturday 26 May 2018

Rais Trump apigwa 'STOP' kublock watu mtandao wa Tweeter



Rais Trump haruhusiwi kumpiga raia ‘Block’ kwenye mtandao wa Twitter kwasababu inakiuka haki yao ya kutoa hotuba na maoni ya bure

Kwa mujibu wa Associated Press, Hakimu wa mji wa New York, Naomi Reice Buchwd amempiga marufuku Rais Trump kuwa’block watu kwenye mtandao wa Twitter hasa wanaomkosoa na kutoa maoni ya kisiasa kwani inakiuka haki yao ya kutoa maoni, Hakimu alisema hakuna afisa wa serikali ikiwemo kamanda mkuu ambaye yupo juu ya sheria

Trump ataruhusiwa kuwa’mute tu watu ambao hataki kuona tweets zao lakini sio kuwa’block kabisa

Kesi ilifunguliwa mwezi wa saba mwaka jana na taasisi ya Knight First amandement ya chuo kikuu cha Columbia na watumiaji saba wa Twitter ambao wanadai kupigwa’block na rais Trump

0 comments:

Post a Comment