Saturday, 8 September 2018

MCHEZAJI WA TOTTENHAM, KOCHA WA WATFORD NA MCHEZAJI WA FULHAM WASHINDA TUZO KWA MWEZI AGOSTI


Mshambuliaji wa timu ya Tottenham, Lucas Moura amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya soka nchini humo kwa mwezi Agosti

Aidha, Kocha wa timu ya Watford, Javi Gracia amechaguliwa kuwa kocha bora kwa mwezi Agosti baada ya timu yake kuanza vizuri ligi hiyo

Kocha huyo amepata tuzo hiyo baada ya kuwashinda makocha Jurgen Klopp(Liverpool), Maurizio Sarri(Chelsea) na Mauricio Pochettino(Tottenham)

Katika tuzo nyingine, mchezaji wa Fulham, Jean Michael Seri amefanikiwa kutwaa tuzo ya goli bora la mwezi Agosti kutokana na goli lake alilofunga kwenye mechi kati ya timu yake na Burnley waliposhinda goli 4-2

0 comments:

Post a Comment