Friday 7 September 2018

Tiger Woods ndani ya kikos cha mashindano ya Ryder Cup


Aliyewahi kuwa mchezaji namba moja kwa ubora katika mchezo wa gofu, Tiger Woods amejumuishwa kwenye kikosi cha Marekani kitakachokwenda kushiriki mashindano ya Kombe la Ryder (Ryder Cup).
Katika mkutano na waandishi wa habari nchini humo, nahodha wa timu hiyo Jim Furyk amesema ni vyema kuongeza wachezaji kwenye kikosi chao ambao wataongeza nguvu na kutoa ushindani.
Sanjari na Woods, wengine walioongezwa ni Phil Mickelson na mchezaji chipukizi, Bryson DeChambeau.

0 comments:

Post a Comment