Wednesday 21 March 2018

Faru pekee mweupe amekufa Kenya



Faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino(Faru Weupe wa Kaskazini) aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na miaka 45
Faru huyo aitwaye Sudan alikuwa akitibiwa kwa muda mrefu matatizo yaliyotokana na kuzeeka kwake katika shamba kubwa la uhifadhi wa wanyama la kituo cha Ol Pejeta


Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinashindwa kupona kutokana na umri wake. Hali yake ilidhohofu sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita


Matabibu wa wanyama kutoka kituo cha uhifadhi wa wanyama cha Dvur Kralove kutoka Jamhuri ya Czech, Ol Pejeta na Shirika la Wanyamapori Kenya waliamua kukatisha uhai wake


Sudan alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya kuangamia


Kwa sasa wamebaki Faru wawili tu aina yake(Najin na Fatu). Faru hao ni wa kike na ni tasa

0 comments:

Post a Comment