Tuesday 6 March 2018

Rais wa Zimbabwe amfurahia kiongozi mpya wa upinzani



Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amempongeza kiongozi mpya wa chama kikuu cha upinzani nchini humo MDC Bw. Nelson Chamisa, kwa kupata nafasi mpya, na kutoa wito wa amani wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu ujao.
Rais Mnangagwa amesema anatarajia kampenzi zitafanyika kwa ushindani, amani na kuwawezesha Wazimbabwe kuchagua kwa uwazi na kidemokrasia. Amesema anatarajia upande wa upinzani utafanya kampeni kwa utulivu bila ghasia, na kuwaruhusu watu wa Zimbabwe kuamua mwelekeo ambao Zimbabwe itaufuata katika miaka mitano ijayo.
Wakati huohuo, aliyekuwa waziri katika serikali ya rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe, Bw. Ambrose Muyinhiri amejiuzulu wadhifa wake wa ubunge akipinga kuondolewa madarakani kwa rais huyo mwezi Novemba mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment