Wednesday 16 May 2018

JPM kuwakabidhi Simba kombe jumamosi hii



Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli, anatarajiwa kuwakabidhi Kombe Mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara VPL ,msimu huu wa 2017/2018 Simba SC, katika mchezo wa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF), Wallace Karia amesema wamemuomba Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za ubingwa wa Simba na Serengeti Boys zinatarajiwa kuanza majira ya saa 8 mchana

Aidha, kabla ya kuwakabidhi Kombe Simba SC, Rais atapokea Kombe la Ubingwa wa CECAFA kutoka kwa Vijana wa Serengeti Boys U17 ambao walilipata wiki chache katika mashindano ya Challenge yaliyofanyika Burundi

Kukabidhi Kombe kwa Vijana hao kwa Rais ni ishara ya maandalizi ya Tanzania katika mashindano ya Vijana ya AFCON mwaka 2019 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano

0 comments:

Post a Comment