Monday 30 April 2018

Simba yazidi kuwapa raha mashabiki wao



Klabu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi baada ya kuirarua klabu ya Yanga goli 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, VPL katika uwanja wa Taifa

Kwa matokeo haya sasa Simba inajiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kunyakua taji la ligi hiyo baada ya kufikisha alama 62 baada ya kucheza michezo 26 na kuendelea kubaki kileleni

Yanga sasa anashuka mpaka nafasi ya 3 akiwa na alama 48 baada ya michezo 24 huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili kwa alama 49 baada ya kucheza michezo 26

0 comments:

Post a Comment