Tuesday 15 May 2018

Ufunguzi wa Balozi ya Marekani,Israel wazua vurugu



Nchini Israel Takribani raia wa Palestina 41 wameuawa na wengine 1,300 kujeruhiwa ambapo 450 kati yao wamepata majeraha ya risasi zilizorushwa na Wanajeshi wa Israeli

Raia wa Palestina takribani 35,000 waliandamana Ukanda wa Gaza wakipinga ufunguzi wa Ubalozi wa Marekani katika mji wa Jerusalem

Makao makuu ya Israeli yalihamishwa kutoka Tel Aviv na kupelekwa Jerusalem na mnamo mwezi Desemba mwaka jana Rais wa Marekani, Donald Trump alitangaza kuutambua mji wa Jerusalem kama Makao makuu ya Israeli

Kati ya waliouawa ni mtoto wa miaka 14 huku mauaji haya yakitajwa kuwa mabaya na yakutisha zaidi tangu mwaka 2014

Wakati haya yakijiri, ujumbe maalum kutoka Ikulu ya Marekani ulioambatana na Mtoto wa rais Trump na Mumewe walikuwa wakishuhudia ufunguzi huo wa ubalozi pamoja na Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu.

0 comments:

Post a Comment