Tuesday, 27 March 2018



Mfanyabiashara wa Dawa za Kulevya Adaiwa kutaka kumhonga shilingi bilioni 1 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ili asikamatwe.

 Kamishna Sianga amesema kuwa Mfanyabiashara huyo wa kemikali bashirifu ambaye hakumtaja jina alitaka kumpa rushwa ya shilingi milioni 400 Kamishna wa Sheria wa Mamlaka hiyo ili aharibu kesi ili asishtakiwe.


Kamishna Sianga alisema pamoja na jitihada za kutaka kuhonga, kigogo huyo na mwenzake walikamatwa mkoani Mwanza.


Alibainisha kuwa waliokamatwa katika usafirishaji wa kemikali hizo ni Mwita Ikohi na Chola Maginga ambao tayari wamefikishwa mahakamani.

Mfanyabiashara wa madwa ya kulevya adaiwa kutaka kutoa rushwa


Mwanadada Johana Konta wa Uingereza amefanikiwa kufuzu raundi ya nne ya mashindano ya tennis ya Miami nchini Marekani baada ya kumshinda Elise Mertens wa Ubelgiji kwa seti ya mbili sifuri yenye alama 6-2 6-1.
Katika raundi ya nne, Konta ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo, atakutana na mchezaji namba nane kwa viwango vya ubora duniani Venus Williams ambaye amefuzu baada ya kumfunga Kiki Bertens wa Uholanzi.

Johana Konta afuzu raundi ya nne



Shirikisho la mpira wa miguu la nchini Uganda FUFA kwa kushirikiana na shirikisho la vyama vya soka barani Afrika CAF, jana limezindua rasmi mradi wa ujenzi wa uwanja wa soka la ufukweni (beach soccer) mjini Entebbe. Mradi huo ambao umegawanyika katika hatua tatu, ujenzi wa sehemu ya kuchezea, ujezi wa majukwaa na ofisi ndogo pamoja na ujenzi wa sehemu za biashara na burudani ndogo kuzunguka eneo hilo, unakadiriwa kuwa utakamilika mwezi mei.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa CAF Amry Fahmy, ambaye alishiriki uzinduzi huo, amesema shirikisho lake limeamua kushirikiana Uganda kukamilisha mradi huo unaokadiriwa kugharimu dola za kimarekani laki mbili sawa na shilingi za Uganda milioni 720, kwa kuwa Uganda wamechaguliwa kuwa wenyeji wa mashindano ya Afrika ya mwezi Mei.

Shirikisho la soka Uganda limezindua rasmi mradi wa Ujenzi wa uwanja

Wataalamu wa masuala ya masumbwi wanasema tangu Anthony Joshua wa Uingereza aanze kushiriki hili ndio litakuwa pambano lake gumu zaidi kuwahi kupigana kwa kuwa atalazimika kuweka rehani mikanda yake pale atakapomkabili Joseph Parker wa New Zealand.
Pambano hili ni muhimu kwa pande zote mbili kutokana na ukubwa wake japo Joshua amesema ndoto yake kubwa ni kuwa na mikanda mitatu ya WBA, IBF na WBC na kufikia rekodi ya Lewis Lennox ya mwaka 2000.
Katika hatua nyingine wataalamu hao wamesifu uwezo wa Bondia Parker ambaye katika mapambano 24 aliyopigana ameshinda yote huku 18 kati ya hayo akishinda kwa knockout.
Pambano hilo linatarajiwa kupigwa siku ya jumamosi katika ukumbi wa ndani wa uwanja wa Principality mjini Cardiff.

Wachambuzi wambeza Anthony Joshua kwa Joseph Parker



Rais Trump ametoa amri ya kufukuzwa kwa wanadiplomasia 60 wa Kirusi, kufuatia Urusi kuhusishwa na shambulio la sumu kwa Jasusi wa zamani raia wa Urusi nchini Uingereza

Tayari nchi za kadhaa za Ulaya zikiwemo Ujerumani, Ufaransa na Ukraine zimetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wa Kirusi katika nchi zao


Viongozi wa EU walikubaliana wiki iliyopita kuwa inawezekana sana Urusi ilihusika katika shambulio la sumu la Sergei Skripal(Jasusi) na binti yake kusini mwa Uingereza


Hata hivyo, Urusi imepinga kuhusika na shambulio hilo

Marekani yawafukuza wanadiplomasia 60 wa Urusi













MAGAZETI YA LEO JUMANNE 27/3/2018

Monday, 26 March 2018

  

Msanii wa muziki wa Hip  Hop nchini Nay Wa Mitego (Mr Nay) ameachia adio ya nyimbo yake mpya ya Amsha Popo.Sikiliza Hapa.
 

Nay Wa Mitego (Mr Nay) – Amsha Popo



Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Machi 25, imemteua Athuman Nyamlani kukaimu nafasi Makamu wa rais wa shirikisho hilo

Nyamlani ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya Michael Wambura kufungiwa maisha kujihusisha na soka


Wambura amefungiwa na kamati ya maadili ambayo imeeleza kumtia hatiani na makosa kadhaa yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa ajili ya malipo ambayo yameelezwa hayakuwa sahihi

Nyamlani achukua nafasi ya Wambura TFF



Polisi wameanza kumchunguza Grace Mugabe juu ya madai ya kuongoza mtandao wa kijangili na usafirishaji haramu wa pembe za ndovu.
 
Grace ambaye ni Mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe pia anatuhumiwa kusafirisha almasi na dhahabu kutoka nchini humo kinyume cha sheria.


Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa, aliagiza uchunguzi wa dharura katika shughuli za Bi. Grace baada ya ushahidi wa 'nguvu sana' uliotolewa na Adrian Steirn, mwandishi wa picha wa Australia.

Grace Mugabe ndani ya tuhuma nzito



 Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM imetengua uteuzi wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi-UVCCM Taifa, Jokate U. Mwegelo kuanzia leo Machi 25, 2018

Kamati hiyo ilikutana kwa dharura leo mchana chini ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu. Kheri Denis James
Sababu za kutengua uteuzi huo bado hazijawekwa wazi

Jokate avuliwa uongozi UVCCM



Wagonjwa wa akili 55 waliokuwa wametenda makosa mbalimbali yakiwamo ya jinai, wameachiwa huru baada ya Mahakama kutowatia hatiani

Profesa Kabudi alisema kifungu cha 219(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, sura ya 20 kinampatia waziri wa sheria mamlaka ya kuwaachia huru wagonjwa wa akili waliotenda makosa ya jinai yakiwamo ya mauaji


Alisema kwa muda mrefu wagonjwa hao walikuwa wakihifadhiwa kwenye taasisi ya Isanga mkoani Dodoma kusubiri amri ya waziri


Aliongeza kuwa “Kutokana na hali ya afya zao za akili kuimarika, niliamua waachiwe huru ili waungane na familia zao kuendelea na matibabu wakiwa nje ya taasisi hiyo.”

Wagonjwa wa akili 33 waachiwa huru










MAGAZETI YA LEO JUMATATU 26/3/2018

Sunday, 25 March 2018



 Kocha Mkuu wa zamani wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji wa Tanzania wanafungwa mechi ngumu kwa sababu ni wazito wa kufanya maamuzi binafsi wanapokuwa uwanjani

Mkwasa ameeleza kuwa tatizo kubwa la wachezaji wa Tanzania ni kutegemea zaidi maelekezo kutoka kwa kocha badala ya uwezo wao wenyewe, hivyo huishia kufanya vibaya kwenye michezo muhimu

Akizungumzia michezo ya kimataifa ya siku za hivi karibuni, Mkwasa amesema Taifa Stars ilipoteza kizembe mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria, ambapo ilifungwa mabao 4-1

Kocha huyo ambaye miaka 2 iliyopita alikuwa akiifundisha Taifa Stars, ametoa wito kwa timu ya Taifa kujiandaa vyema kwa ajili ya mchezo mwingine dhidi ya DRC, utakaochezwa mnamo Machi 27 jijini Dar es Salaam ili kuepuka kurudia makosa.

Mkwasa awavaa Taifa Stars adai wanachelewa sana kuchukua maamuzi



 Sherehe ya kifahari ya binti wa Bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote aitwaye Fatima Dangote, yazua gumzo nchini humo kutokana na kuhudhuriwa na watu mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali duniani akiwemo Bilionea kutoka Marekani, Bill Gates.

Naye Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete alikuwa ni miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria katika sherehe hiyo ya kihistoria.

Wengine walioudhuria ni pamoja na mke wa Rais wa sasa wa Nigeria, Hajiya Aisha Buhari; Makamu wa Rais, Osinbanjo; Spika wa Bunge, Magavana na Watu wengine mashuhuri wakiwemo wasanii na wafanyabiashara wakubwa.

Tafrija hiyo ya mapokezi baada ya ndoa (reception) kati ya Fatima na mumewe ambaye ni mtoto wa Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, Jamilu Abubakar, ilifanyika jana Ijumaa katika Jiji la Lagos.

Harusi ya Binti wa Dangote yakutanisha matajiri,watu mashuhuri









MAGAZETI YA LEO JUMAPILI 25/3/2018

Saturday, 24 March 2018



Mwanamitindo maarufu asiwe ishiwa na vituko kutoka Marekani,Black Chayna amewajia juu watu wanaomsema juu ya kuwa katika mahusiano na mpenzi wake mwenye umri mdogo.

Utata ulizuka baada ya mwanadada huyo Blac Chyna mwenye umri wa miaka 29 alivyomuweka kupitia ukurasa wa Instagram (kibenten) wake YBN Almighty Jay mwenye umri wa miaka 18.


"Hakuna tatizo kuwa na mahusiano na mtu mwenye umri mdogo kikubwa awe anajielewa tu," alisikika Blac Chyna.

Blac Chyna awavaa wanaomsema kutembea na "Kibenten"



Staa wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Marekani frenchmontana anatarajia kufungua hospital nchini Uganda ambayo alitolea ahadi mwaka jana.


Msanii huyo ambaye kwasasa amejitolea sana katika kuhakikisha kuwa Huduma za Afya zinafika vijijini nchini Uganda ni kutokana na ushirikiano aliopewa kutoka kwenye moja ya kazi zake alizofanya kama nyimbo ya "unforgettable".


Kupitia ukurasa wake wa Tweeter aliandika kuwa .
" Ni naamini malengo yangu yametimia kwa nchi ya Uganda hivyo nitakwenda kwaajili ya ufunguzi wa hospitali.

FRENCH MONTANA KATIKA UZINDUZI YA HOSPITALI UGANDA



Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, imesema Mahakama za Tanzania zilitenda haki na kukiuka pia kwa upande mwingine katika hukumu ya Babu Seya na Papii Kocha.
Mahakama imewaruhusu Babu Seya pamoja na Papii Kocha kuwasilisha hoja ya kuomba fidia kulingana na haki zao ziliokiukwa


Mfano wa haki iliyokiukwa ni kukaaa mahabusu kwa siku 4 bila kufahamishwa makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea


Pia wawili hao waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama waliwaingilia Watoto wale ambao upande wa Jamhuri ulidai waliambukizwa magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa


Maombi hayo yanapaswa kuwasilishwa ndani ya kipindi cha siku 30

Kesi ya Babu Seya yafikia ukingoni









MAGAZETI YA LEO YA JUMAMOSI 24/3/2018