Saturday, 8 September 2018


Mshambuliaji wa timu ya Tottenham, Lucas Moura amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya soka nchini humo kwa mwezi Agosti

Aidha, Kocha wa timu ya Watford, Javi Gracia amechaguliwa kuwa kocha bora kwa mwezi Agosti baada ya timu yake kuanza vizuri ligi hiyo

Kocha huyo amepata tuzo hiyo baada ya kuwashinda makocha Jurgen Klopp(Liverpool), Maurizio Sarri(Chelsea) na Mauricio Pochettino(Tottenham)

Katika tuzo nyingine, mchezaji wa Fulham, Jean Michael Seri amefanikiwa kutwaa tuzo ya goli bora la mwezi Agosti kutokana na goli lake alilofunga kwenye mechi kati ya timu yake na Burnley waliposhinda goli 4-2

MCHEZAJI WA TOTTENHAM, KOCHA WA WATFORD NA MCHEZAJI WA FULHAM WASHINDA TUZO KWA MWEZI AGOSTI

Friday, 7 September 2018


Aliyewahi kuwa mchezaji namba moja kwa ubora katika mchezo wa gofu, Tiger Woods amejumuishwa kwenye kikosi cha Marekani kitakachokwenda kushiriki mashindano ya Kombe la Ryder (Ryder Cup).
Katika mkutano na waandishi wa habari nchini humo, nahodha wa timu hiyo Jim Furyk amesema ni vyema kuongeza wachezaji kwenye kikosi chao ambao wataongeza nguvu na kutoa ushindani.
Sanjari na Woods, wengine walioongezwa ni Phil Mickelson na mchezaji chipukizi, Bryson DeChambeau.

Tiger Woods ndani ya kikos cha mashindano ya Ryder Cup



Timu ya taifa ya Wales imeifunga bila huruma timu ya taifa ya Ireland magoli 4-1, Gareth Bale amefunga moja kati ya magoli hayo manne na kufikisha jumla ya magoli 30 katika timu hiyo.
Uholanzi nayo imeichezesha mchakamchaka Peru na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Ureno wakicheza bila Christiano Ronaldo, wamelazimika kumtumia Pepe kusawazisha goli dakika ya 32 baada ya Ivan Perisic kutangulia kuwafungia Croatia katika dakika ya 18. Hadi mwisho wa mchezo, Ureno imetoka sare za Croatia ya goli 1-1.

Matokeo ya michezo ya kirafiki ya kimataifa Ulaya

Thursday, 6 September 2018



Makocha wa timu kubwa barani Ulaya wamekitaka chama cha mpira barani humo (UEFA) kufanya mabadiliko ya kanuni ya faida ya magoli ya ugenini katika michuano ya ligi ya Ulaya (EUROPA LEAGUE).
Makocha hao pia wamependekeza msimu wa usajili uhitimishwe kwa wakati mmoja katika ligi zote kubwa za Ulaya.
Kanuni ya faida ya goli la ugenini ilianzishwa mwaka 1965 kama mbadala wa kurusha sarafu ama kuandaa mechi ya marudiano katika uwanja huru (usio wa timu yeyeote shindani) pale ambapo matokeo ya mechi mbili za timu zinazoshindana yanapokuwa sare.
Pia makocha hao wamependekeza kuwa dirisha la usajili limalizike kwa wakati mmoja katika ligi zote kubwa barani humo.

Makocha UEFA Wataka sheria mpya



Imefuzu kucheza Fainali hizo baada ya mpinzani wake Afrika Kusini kuwasilisha kwa CAF barua ya kujiondoa katika mashindano

Fainali hizo za Afrika zinatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 9 - Desemba 14, 2018 na kushirikisha nchi 8

Timu hiyo ilikuwa kambini kujiandaa na mchezo huo(dhidi ya Afrika Kusini) uliokuwa uchezwe Jumapili Septemba 9, 2018

TIMU YA TAIFA YA SOKA YA UFUKWENI YA TANZANIA IMEFUZU KUCHEZA FAINALI ZA AFRIKA NCHINI MISRI



Eminem anakamata nafasi ya kwanza wiki hii Billboard 200.

Rapper Eminem anazidi kuzihirisha yeye ni Rap God katika kizazi hichi kipya cha kina Travis Scott na Drake, kwa kutabiriwa kushika namba moja katika chat za Billboard 200 wiki hii kwa makadilio ya mauzo nakala 365,000 mpaka 385,000 ndani ya wiki moja katika album yake mpya "Kamikaze" aliyotoa ghafla kwa kushitukiza bila promo.
.
.

Eminem azidi kuwa tishio



Mwanamziki kutoka Canada, Drake anaendelea kuvunja na kuweka record mbalimbali za mziki nchi Marekani, sasa Drake amevunja record ya muda mrefu ya Usher kama msanii wa kiume anaengoza kwa kushika namba 1 katika chat za Billboard Hot 100 kwa kufisha jumla ya wiki 47 katika nafasi ya kwanza kupitia nyimbo zake "God's Plan", "Nice For What" na "In My Feelings".

Drake avunja record ya Usher Raymond.



Kijana huyo ambaye ni mgonjwa wa akili alifanyiwa upasuaji huo katika hospitali teule ya Missenye, Mugana na kukutwa pia na viberiti vya gesi, mfuko, vitambaa na ganda la limao

Dkt. Eliud Nyonyi aliyeshiriki kumfanyia upasuaji mgonjwa huyo, Eliud Novart(25) amesema baada ya vitu hivyo kutolewa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri
 

Mganga Mkuu wa Missenye, Dkt. Hamis Abdallah alisema mgonjwa alifikishwa katika Hospitali ya Mugana baada ya kupatiwa rufaa na Hospitali ya Nyakahanga, wilayani Karagwe

Gumzo: Akutwa na Viberiti na vitambaa tumboni

Wednesday, 5 September 2018



Dully Sykes pamoja na @harmonize_tz waachia video ya ngoma yao mpya #Kadamshi 🎬🎬.
 

ITAZAME HAPA

Ngoma mpya ya Harmonize & Dully Sykes- KADAMSHI VIDEO



Kocha  wa Manchester United, Uingereza, Jose Mourinho amekubali adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi.
Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa Novemba 4 mwaka jana na mahakama ya Pozuelo de Alarcon ya mjini Madrid imehitimishwa baada ya uchunguzi na kwamba Mor ana hatia ya makosa mawili tofauti yenye vifungo vya miezi sita kila moja.
Mahakama hiyo pia inatarajiwa kutoa uamuzi wa aidha kumpeleka kocha huyo wa Manchester United jela, au kumweka katika msamaha wa wakosaji wa mara ya kwanza na kumtaka alipe deni la kodi na fidia ya usumbufu.

Kocha Jose Mourinho kwenda jela mwaka mmoja kwa kukwepa kodi



 Kupitia ukrasa wake wa Instagrama mwanadada Wema avunja ukimya na kuandika maneno mazito juu ya Mange Kimambi.
 @wemasepetu Kama maneno mkuki, Lenga unifyatulie... Kusanyana mashabiki, waje wakusaidie.... Imara sibabaiki.... Tena nitazame ndie mie.....
To whom it may Concern.... Kubambwa mbambwe muanze kusema yangu.... Nimechoka sasa.... Kwani aliefurahia ni mimi peke yangu.... Yaani wewe dada mpaka huwa nakuskitikia wallahy.... Ebu mniache basi... Ndo mshakutwa tena Red Handed.... .
.
.
Red Handed Nako K... Defence hamna kiukweli... Ndo ipo hivyo... Pambaneni na hali zenu please.... And Yoooou.... Kuwa mshauri mzuri basi kwa mdogo wako....
.
.
.
Miaka Kumi nayo K... 😂😂😂😂😂😂😂😂 Umebakia kusema Nyumbu Nyumbu... Smh... Come up with something New Pleaseeee.... Wewe ushakuwa mtu mzima sasa.... Set an Example..... Mxxxxxxxxiuuue .... Mtu Mzima Ovyooooooooooo..... Fanyeni mtoe na Vn zangu za Kuloga basi... Eti leo mnasema vya Muna kusema na wakati aliulizwa akakataa.... Mna wazimu nyie eeh.... Wewe huwa nakuonaga ni mkubwa basi nikupe heshima kama dada ila hustahili heshima hata kidogo mbwa wewe.... Baki kwenye mipaka yako hangaika na maisha yako.... Usimdanganye huyo mtoto mchawi kuwa anaweza kuwa mimi hata siku moja.... Hawezi na hatokaa aweze.... Mmedhalilika na ndo itabaki kuwa hivyo..... Aibuuuuuu saaaaaanaaaa Mungu wangu.... Yaani hata azikiri UCHI hawezi.... Mxxxxxxiiiuueee
.
.
.
Mmebambwaaaaaaaa ..... Tena Mmebambwaaaaa Vizuri..... Aibuuuuuuuuuu..... Mambo mmeyatindinganya huko mnimalizie hasira mie... Eti Wema Wema.... Si sina mvuto mimi... Nini nimekukaa kooni mbwa wewe.... Sikuheshimu.... Sikupendi na Nataka uniache na Maisha yangu hayakuhusu.... .
.
.
.
Tukio la leo ni zito sana.... Hata mimi ningekuwa Hoves.... 😒😒😒
.
.
.
Oh nd By the way.... Yes Mimi Ni Tasa SO WHAT....????

Wema Sepetu amshushia kichambo Mange kimambi



Nicki Minaj bado ana kinyongo na Travis Scott kwa kumpita katika mauzo ya album yake ya "Queen" na kumfanya ashindwe kushika namba 1 katika chat za Billboard 200. Nicki wakati anafanya interview na kipindi cha #hellen alifunguka na kusema anatamani kumpiga usoni Travis kwa kumpita katika mauzo.

Nicki Minaj anamtamani Travis Scott.



Majina 100 toka mataifa 26 ya Afrika yametajwa na mtandao wa Africa Youth Awards kwenye list ya mwaka 2018 ya vijana 100 wenye ushawishi mkubwa.

Kati ya hao 100, majina ya Watanzania 12 yametajwa pia: Ali Kiba, Millard Ayo, Mbwana Samatta, Faraja Nyalandu, Herieth Paul na wengine.

Huu ni mwaka wa tatu wa tuzo hizo mahususi kwa vijana kwenye nyanja kama: Siasa, Harakati, Ujasiriamali, Burudani, Washawishi wa mtandaoni na Wanamichezo ambao wanatangaza sura ya Afrika kwa muonekano chanya kwenye ramani ya dunia.

Millard Ayo,Faraja Nyalandu,Ali Kiba,Samatta vijana wenye ushawishi Afrika

Tuesday, 4 September 2018

  •  
    Mahakama ya kidini(Kiislamu) nchini Malyasia imewahukumu Wanawake wawili kuchapwa fimbo 6 kila mmoja kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja
    -
    Adhabu hiyo imetekelezwa kwenye Mahakama ya Sharia iliyopo katika Jimbo la Terengganu huku takribani Watu 100 wakishuhudia
    -
    Watetezi wa Haki za Binadamu wamelaani vikali kitendo hicho na kukiita ni cha kikatili na cha kidhalilishaji
    -
    Hata hivyo kwa upande wa Mahakama umetetea adhabu hiyo na kuongeza kuwa imetolewa hadharani ili iwe onyo na fundisho kwa wengine

WACHAPWA VIBOKO KWA KUJIHUSISHA NA USAGAJI


Mchezaji bora namba moja wa zamani kwa upande wa wanawake, Serena Williams amefanikiwa kutinga robo fainali ya mashindano ya US Open kwa ushindi wa seti (6-0, 4-6, 6-3).
Kaia Kanepi aliyetinga hatua hiyo bila kupoteza seti hata moja alishindwa kuhimili uwezo wa Williams licha ya kushinda kwenye seti ya pili kwa 6-4 hali iliyopelekea mchezo huo kwenda kwenye raundi ya tatu.
Serena aliyemtoa dada yake Venus kwenye raundi iliyopita hakusita kuonyesha furaha yake baada ya mchezo huo na kusema mpinzani wake alikuwa mchezaji hodari.
Mmarekani huyo atakutana na Karolina Pliskova kwenye robo fainali na iwapo atashinda huenda akakutana na bingwa wa zamani wa mashindano hayo Maria Sharapova ambaye pia ametinga robo fainali baada ya ushindi wa seti mbili mfululizo za 6-3, 6-2) dhidi ya Jelena Ostapenko.

Serena Williams azidi kuonesha ubabe ,atinga robo fainali


Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Mohamed Salah ndio wachezaji watatu wa mwisho ambao watawania tuzo la mchezaji bora wa FIFA mwaka huu.
Hakuna mchezaji yeyote aliyekuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda kombe la dunia.
Jopo la wataalamu wa FIFA waliunda orodha ya wachezaji 10 kwa kila tuzo huku manahodha wa timu za taifa, waandishi wa habari na mashabiki wakimchagua mshindi kila kundi likiwa na asilimia 25 ya kura.
Washindi watatangazwa tarehe 24 Septemba huko Royal Festivan mjini London.

Ronaldo, Modric na Salah kuwania tena tuzo mchezaji bora FIFA


Ameahidi hayo leo wakati akishuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Meli mpya na chelezo katika Ziwa Victoria, ujenzi utakaogharimu Tsh. Bilioni 88. 76

Wafanyakazi hao wanaodai malimbikizo ya mishahara ya takribani miezi 27 wamehimizwa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi vinginevyo watazitapika fedha hizo

Aidha, Rais Magufuli amemsifia Kaimu Mkurugenzi wa Marine Services kwa kazi nzuri na kumshangaa Waziri wa Uchukuzi kutompa Ukurugenzi kamili

RAIS MAGUFULI AAHIDI KUTOA TSH. BILIONI 3.7 NDANI YA WIKI 2 KWA WAFANYAKAZI WA MARINE SERVICE



Mamlaka nchini Kuwait zimelifunga duka moja la kuuza Samaki baada ya mmiliki wake kubainika kuwalaghai wateja wake juu ya ubora wa Samaki wake
-
Sakata hili limeibuka baada ya Mwanamke mmoja kuweka video katika mtandao wa Facebook akitoa jicho bandia la Samaki aliyemnunua

DUKA LAFUNGWA BAADA YA MMILIKI WAKE KUWAWEKEA SAMAKI MACHO YA BANDIA ILI WAONEKANE ''FRESH''

Sunday, 2 September 2018


Mbunge wa Kyadondo East na mwanamuziki wa Dance Hall kutoka nchini Uganda Bobi Wine mapema Leo kupitia ukurasa wake wa Tweeter ameandika kuwa amefika salama nchini Marekani ambapo anatarajia kuendelea na matibabu zaidi.

Hata hivyo Bobi Wine ameandika kuwa muda ukifika ataeleza mambo yote yaliyomtokea kipindi anateswa.

Bobi Wine afika salama nchini Marekani,aahidi kusema kilichomtokea

Saturday, 1 September 2018


.
Eminem ameishitukiza Dunia kwa kuachia album ghafla ikiwa ni miezi 8 imepita tangu alipoachia album ya "Revival" ambayo ilikamata nafasi ya kwanza katika Billboard 200. Cover ya album inafanana na cover ya album ya "Licensed to III" ya kundi la zamani la Beastie Boys mwaka 1986.
.
.
Album hiyo inachukua muda wa dakika 45 tu kuisikiliza ikiwa na jumla ya nyimbo 13, ndani yake kawashirikisha Jessie Reyes, Joyner Lucas, na Royce Da 5'9". Kwenye production imehusika mikono ya Dr Dre na Eminem mwenyewe aka Slim Shady kwa kushirikiana na Mike Will Made It, Tay Keith na Boi-1da
.
.
Album ya "Kamikaze" inakuwa album ya 10 kwa Eminem, pia katika album hiyo track mbili ni voicemail kati ya Eminem na meneja wake Rosenberg. Track moja Rosenberg anaongea baada ya kuisikiliza album ya "Kamikaze" na kumuuliza maswali Eminem kuhusu "Kamikaze"
.
“Are you really going just to deride everybody who, you don’t like what they have to say about you or the stuff you’re working on? I don’t know if that’s really a great idea, it’s like what’s next, ‘Kamikaze 2,’ the album where you reply to everybody who didn’t like the album that you made replying to everybody that didn’t like the previous album? It’s a slippery slope, I don’t know if it’s really a good idea.”
.
.
Neno "Kamikaze" ni neno la kipajani na maana yake ni upepo wa mungu. Pia katika album ya "Kamikaze" kuna nyimbo ambayo imetumika kama soundtrack katika Movie mpya ya "Venom" ambayo bado haijaachiwa. Na hii ndio tracklist ya album ya "Kamikaze"
.
#1 The Ringer
#2 Greatest
#3 Lucky You (feat. Joyner Lucas)
#4 Paul – Skit
#5 Normal
#6 Em Calls Paul – Skit
#7 Stepping Stone
#8 Not Alike (feat. Royce Da 5’9′)
#9 Fall
#10 Kamikaze
#11 Nice Guy (feat. Jessie Reyez)
#12 Good Guy (feat. Jessie Reyez)
#13 Venom – Music from the Motion Picture
.

Surprise! Eminem just dropped a new album .